Covenant Protestant Reformed Church
Bookmark and Share

Imani Ya Kaledonia

 

Sisi, basi, tukiwafuata baba zetu watakatifu, sote kwa ridhaa moja, twafunza watu kukiri Mwana yule mmoja, Bwana wetu Yesu Kristo, yeye mkamilifu katika utatu na pia katika ubinadamu; Mungu kweli na binadamu kweli, mwenye roho na mwili zote kamili kawaida; hususan na Baba kulingana na utatu, hususan kama sisi kibinadamu; katika vyote kama sisi, bila dhambi, wa pekee wa Baba kabla ya nyakati kulingana na utatu, na siku hizi za baadaye, kwa ajili yetu na wokovu wetu, mzaliwa wa bikira Maria, mama ya Mungu, kibinadamu; Kristo mmoja yule, Mwana, Bwana, wa pekee, atambuliwe katika asili mbili, bila kuchanganyikiwa, kugeuzwa, kugawanywa, kutengwa; tofauti katika asili isiwe nafasi ya kubatilisha hali ya umoja, bali hulka ya kila asili ikihifadhiwa na kukubaliana katika mmoja na katika dutu moja, si kugawanywa au kutengwa kuwa wawili, bali mwana huyo mmoja, pekee, Mungu Neno, Bwana Yesu Kristo; vile manabii tokea mwanzo (wamefunza) kumhusu, na Bwana Yesu Kristo ametufunza, na imani ya baba watakatifu tuliyoachiwa.