Covenant Protestant Reformed Church
Bookmark and Share

Kristo, Arbuni Yetu

Rev. Angus Stewart

 

Mnajua arbuni ni nini. Arbuni ni malipo ili kuwezesha kufunguliwa kwa watekwa-nyara. Mmesikia visa vingi vya wateka-nyara au wagaidi wakishika au wakifunga watu. Huwa wanadai arbuni: “Ukitulipa (kiwango cha fedha), tutamwachilia huru mpendwa wako.”

1 Timotheo 2:6 husema kuwa Bwana Yesu “alijitoa kama sadaka/arbuni.” Msalaba wa Kristo sio tu arbuni ya ki-ishara; ni arbuni halisi. Kuna watekwa-nyara halisi katika ufungo halisi; chini ya dhambi (Warumi 3:9), chini ya kuhukumiwa kwa sheria (19), chini ya laana ya sheria (Wagalatia 3:10), kwa ufungo wa mauti, chini ya uwoga wa mauti (Waebrania 2:15), ndani ya utumwa wa Shetani (Waefeso 2:2), katika ufungo kwa dunia na chini ya uwoga wa kuzimu.

Kuna malipo ya arbuni halisi kwa ajili ya watekwa-nyara halisi katika ufungo halisi. Hii ni arbuni yenye dhamani isiyopimika: Mwana halisi wa Mungu katika ubinadamu, aliyekuwa mtiifu kila mara na hakuwahi tenda dhambi. Alibeba adhabu yetu kwa ajili ya dhambi zetu kwa kujitolea kama sadaka/arbuni, akikubali kutii Baba yake na kwa upendo usiopimika kwetu, kama malipo ya dhambi zetu kwa hiari.

Arbuni hii halisi hulipwa kwa watekwa-nyara halisi katika katika ufungo halisi kwa mteka-nyara halisi. Arbuni hulipwa kwa Mungu na sio kwa Shetani, tofauti na tetesi ya kitambo kuwa hulipwa kwa Shetani kuhusu upatanisho wa Kristo. Hiyo arbuni hulipwa kwa yule Mmoja jinsi toleo la Kristo na sadaka hufanywa. “Kupitia Roho wa milele,” Kristo “alijitolea bila mawaa kwa Mungu” (Waebrania 9:14). “Kristo pia alitupenda, na amejiltolea kwa ajili yetu kama toleo na sadaka kwa Mungu kama manukato” (Wa-efeso 5:2). Arbuni hulipwa kwa Muweza-yote, anayezingatiwa kama mtoaji wa sheria, mtawala na hakimu, Mwenya-haki na Mtakatifu tuliyemkosea, ili kuridhika kuwekwe kwa sheria na hulka zake takatifu.

Tambua uhusiano kati ya mpatanishi na arbuni. Bwana wetu Yesu Kristo ni mpatanishi na tena ni arbuni yetu,maana yeye ni mpatanishi aliyejitolea kama arbuni yetu, vile Mtume asema, “Kwa kuwa kuna Mungu Mmoja, mpatanishi mmoja kati ya Mungu na binadamu, Yesu Kristo mwenyewe; aliyejitolea kama arbuni” (1 Timotheo 2:5-6). Ukweli wa “mpatanishi mmoja” hutuelekeza kwa arbuni yake moja. Kwa nini? Maana mpatanishi kati ya Mungu na binadamu aweza tu kutoa uadui kati yetu na kuwezesha ushirika kati yetu kwa misingi wa arbuni yake kwetu kutoka kwa hukumu ya utakatifu wa Yehova.

Tofauti na maandiko, kuna mfumo mzinifu wa ukatoliki wa Kirumi. Roma hufunza watu kuwa inapasa tuombe kwa na kuwapitia waamini-watakatifu, na hii huwafanyisha wapatanishi, tofauti na ukweli kuwa Kiristo ndiye “mpatanishi mmoja.” Pia, kama watu wangalichukua kutoka kwa hazina ya matendo mema ya waamini-watakatifu, inayowafanya watoe sehemu ya arbuni yetu. Roma hufunza kuwa Maria (siye kama mwanamke mtakatifu katika Bibilia, bali mungu katika fikira) kama muombezi wa watu, maana watu wapaswa kuomba kwa na kumpitia Maria. Tena na tena, Maria hufikiriwa na huongelewa kama mwokozi-mwenza anayelipa arbuni kwa ajili ya watenda dhambi. “Mpatanishi Mmoja” wetu “kati ya Mungu na binadamu, Yesu Kristo mwenyewe … alijitoa kama arbuni/kwa ajili ya wote” (5-6). Mnajua wafuasi wa Armini wanavyofanya na maneno “kwa ajili ya wote.” Wakifuata tetesi yao kuhusu kukosa uwezo wa kujiokoa kwa binadamu (Warumi 3:11) (maana wanafunza kuwa binadamu ana uhuru na huweza kumchagua Kristo na wokovu wake Kristo) na kukataa kwao kuhusu uchaguzi wa milele wa Mungu na kukataliwa kwa wengine (Warumi 9:11-24), roho asiyeshindwa (Waefeso 1:19) na subira ya waaminio halisi (Yohana 10:27-30), hudai kuwa Kristo alilipa gharama ya arbuni kwa kila mmoja, kichwa kwa kichwa. Wananukuu “kwa ajili ya wote” kwa nderemo, kana kwamba hiyo huthibitisha madai yao. Ukiwauliza thibitisho kuwa “wote” humaanisha kila mmoja aliyeishi au ataishi. Hawatoi thibitisho lakini wanazidi bila aibu. Ukitoa maandiko katika Bibilia - nyingi yao! - penye neno “wote” halimaanishi kila mmoja kichwa kwa kichwa na tena uwaulize thibitisho kama hilo neno humaanisha vile wanavyodai … Tena thibitisho halitolewi.

Ukiwauliza kama Yesu alikufia haswa wanaotenda dhambi isiyosameheka, ambao tumeamriwa tusiwaombee (Mathayo 12:32; 1 Yohana 5:16). Ukiuliza sababu Kristo alimwaga damu yake ya dhamana kwa ajili ya wale hawaokoleki kutoka kuzimu (Luka 16:26). Kwa nini Kristo alipe gharama ya dhambi kumwokoa Mpinga-kristo, mwana wa kuzimu, ambaye uharibifu wake wa millele umewekwa na kutabiriwa (2 Wathesalonike 2:3, 8; Ufunuo 19:20; 20:10)? Wafuasi wa Armini “hukosa … bila kujua maandiko, wala nguvu wa Mungu” (Mathayo 22:29). Kwanza, hawajui nguvu ya Mungu katika arbuni ya Kristo. Bwana Yesu alilipa gharama/arbuni, lakini kulingana na imani ya Armini, haikuokoa wengi waliolipiwa hiyo gharama. Yehova alipata arbuni lakini hakuachilia huru wengi waliolipiwa gharama! Kumbuka hii arbuni ilikuwa halisi iliyotolewa na kukubaliwa miaka elfu mbili ilyopita (2,000).

Sasa imani ya Armini hudunisha nguvu (na hekima) ya Mungu mwana, aliyelipa arbuni, na nguvu (na uaminifu) ya Mungu Baba, aliyekosa kuwachilia huru wale aliopata arbuni yao. Tena, wafuasi wa Armini hufikiri nini kuhusu yesu kama mpatanishi? Kosa kubwa! Ni mpatanishi asiyeweza maana hafui dafu kwa kuwarejesha wengi aliowapatanisha kwa Mungu, maana wengi wako katika uadui na Yehova katika dunia hii na ile ijayo. Pili, tetesi ya ki-Armini ya arbuni kwa kila mmoja huashiria kuwa hawajui maandiko, maana kuna maandishi mengi yanayothibitisha upekee wa arbuni ya Yesu (kwa mfano Isaya 53:10-12; John 10:11, 15; 15:13-14; Waefeso 5;25). Zaidi, 1 Timotheo 2:6 lazima lielewe vile ipasavyo. “Watu wote” katika aya ya kwanza (1) huelezwa kama aina yote ya binadamu, hasa hapa, “Wafalme” na “wote katika mamlaka” (2). Na sasa lazima tuwaombee, hata wakiwa wenye ubaradhuli au wakitudhulumu (1-2). Mungu hupenda kuokoa watu wote (4), watawala, na hakuna mwokozi ye yote au wokovu mbadala kwa watawala na mahakimu, kwa kuwa kuna “mpatanishi mmoja” (5) aliye “jitolea kama sadaka/arbuni kwa wote” (6). Ahsante kwa Mungu mwenye utatu, kwa Kristo, mpatanishi wetu pekee na arbuni yetu, tumaini letu pekee! Bwana awe nanyi!