Covenant Protestant Reformed Church
Bookmark and Share

Kumjua Mungu Wa Kweli

Mchungaji: Steven Houck

 

Uzima Wa Milele

Je! Wamjua Mungu wa KWELI? Sio Mungu anaye fikiliwa katika mawazo ya Binadamu,lakini ni Mungu Aliyenenwa katika Biblia? Je! wamjua na fahamu za ndani ili ukampende na kumtumikia? Hili ni swali nyeti. Bibilia yafundisha hivi, Uzima wa milele ni kumjua Mungu pamoja na mwanawe Yesu Kristo. Yesu asema, “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana Mtakatifu 17:3). Kama utakuwa na uzima wa milele na huishi na Mungu milele Mbinguni, ni lazima humjue Mungu na mwanawe Yesu Kristo.

Ikiwa una hamu ya kumjua Mungu wa kweli, basi tafakali yafuatayo:

 

Mungu Wa Kweli

Bibilia yafundisha kuwa Mungu ni Mkuu na Mwenya Utukufu. Yeye ni Mungu aliye juu.” BWANA ni Mkuu juu ya mataifa yote, na utukufu wake ni juu ya Mbingu. Ni nani aliye mfano wa BWANA, Mungu wetu aketiye juu, Anyenyekeaye kutazama Mbingu na duniani” (Zaburi 113: 4-6). Hakuna aliye kama Mungu kwa ukuu. Hakuna kiumbe dunianikote ambacho kitalinganishwa na Mungu.Mungu ni mmoja katika Utatu Takatifu. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Mungu hana mwanzo wala mwisho, anajitegemea, habadiliki nay u juu ya vyote. Ni mwenye nguvu, mwenye hekima sote na yuko kila mahali. Mungu wa mbingu na nchi ni Mtakatifu, mwenye haki,na adili. Ni mwingi wa upendo, neema na kweli. Ni Mkuu hata utukufu wake wapiti mataifa yote na hata juu ya mbingu. Hatuwezi kulinganishwa na Yeye. “Mataifa yote huwa kama si kitu mbele zake,huhesabiwa kwake kuwa dunia si kitu, na ubatil” (Isaya 40:17).

Ukuu wa Mungu waweza kudihilika katika kazi za ajabu Amefanya. Bibila yafundisha kuwa, Mungu ndiye Muumba wa vyote. Tuna soma hivi, “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi” (Mwanzo 1:1). Ulimwengu haukujitokeza kwa njia na fikila za mwanadamu. Ulimwengu uliumbwa na Mungu kwa siku sita. Mungu Alitamka tu Neno Lake lenye uwezo na Ulimwengu ukaumbwa. “Kwa neon La BWANA mbingu zilifanyaika, na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake … Maana Yeye Alisame, na ikawa Na Yeye aliamru ikasimama” (Zaburi 33: 6, 9). Mungu ni Mkuu hata akaufanya ulimwengu bila chochote. Bibila yatufundisha, “Kwa imani twafahamu kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neon la Mungu, hata vitu vilivyo dhahiri” (Waebrania 11:3). Kila kiumbe sis tukiwemo, uhai wake umetokana na Mungu.

Mungu si muumbaji tu wa ulimwengu,bali pia Yeye ndiye Anayeusitili ulimwengu. Anaushikilia ulimwengu ndipoza unaendelea kuwepo. Ezra akasema, “Wewe ndiwe BWANA, we we peke yako,wewe ulifanya mbingu, mbingu za mbingu, pamoja na jeshi lake lote, dunia na vyote vilivyomo, bahari na vitu vyote vilivyomo, nawe unavihifadhi vitu hivi vyote na jeshi lake la mbingu lakusujudu wewe”(Nehemia 9:6). Bila nguvu za kuhifadhi za Mungu, ulimwengu haungekuwepo. Ulimwengu haungesimama peke yake. Uliumbwa na Mungu na kuwepo kwake kunahitaji Mungu.

Hautakuwa chochote wala hutafanyachochote bila Mungu kukushikilia kwa uwezo wake. Mungu “kwa maana Yeye Ndiye anawapa wote uzima na pumzi na vitu vyote … kwa maana ndani yake twaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu …” (Matendo ya Mitume 17:25, 28). Hatutakwenda bila uweza na nguvu za Mungu. Ukuu wa Mungu haunekani tu kwa uumbaji wa ulimwengu kwa nguvu zake,bali pia kwa utawala wake ulimwenguni. Mungu Ndiye Mtawala wa ulimwengu. “BWANA ameweka kiti chakecha enzi Mbinguni,na ufalme wake unavitawala vituvyote” (Zaburi 103:19). Mungu “mwenye uweza peke yake, Mfalme wafalme, Bwana wa mabwana” (1Timotheo 6:15). Yeye si Mungu mdhaifu ambaye mapenzi yake yataadhiliwa na kiumbe chochote. Yeye ni Mfalme wa milele Ambaye anatawala vitu vyote, hata sisi. Anaitawala vitu vyote vya ulimwengu na kuleta yale ambayo ame yapanga kwa uweza wake wa milele kwa ulimwengu na kila mtu. Yeye “Ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake” (Waefeso 1:11). Mungu ndiye mtawala na Mfalme wako.

Hivyo hakuna kiumbe ulimwenguni kote ambacho hakimuhitaji Mungu. Sisi sote twamuhitaji Mungu. Maisha yetu yamtegemea Mungu wa kweli.Hata hivyo, Mungu alikuumba kwa utukufu wake. Bibilia yamzungumzia Mungu, “… kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikwako navyo vikaumbika” (Ufunuo 4:11). Hatukuumbwa kwa starehe zetu wenywewe. Hatukuumbwa tu kwa ajili ya kuishi, bali kwa mapenzi na utukufu wa Mungu.

 

Hitaji La Mungu

Kwa kuwa Mungu ndiye Muumbaji mkuu na utukufu, mhifadhi,na mtawala wa ulimwengu, Anasta hili dhahadima na heshima kutoka kwetu. Tunasoma hivi katika Biblia,” umestahili wewe Bwana wetu na Mungu wetu,kuupokea utukufu na heshima na uweza kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote …” (Ufunuo 4:11). Katika mambo yote Mungu amefanya amejionyesha kuwa wa ajabu na wa pekee, Ambaye mbele zake twatetemeka. Mungu atuhitaji tumwogope na kumpa heshima. “Nchi yote naimwogope Bwana, wote wakao duniani na wamche” (Zabauri 33:8). Hili si jambo la kuchagua, bali ni amri ya Mungu. Tunahitajika kimaadhili kuwa na heshima kwa muumba wetu.

Heshima ambayo Mungu anahitaji inapatikana katika kuabudu, shukrani, na huduma. Kama kiumbe wa Mungu lazima humwabudu Yeye. “Njooni twaabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba” (Zaburi 95:6). Mungu anakuhitaji humkili kama Muumba, Mhifadhi na Mtawala kwa kuinama mbele zake na kwabudu, kwabudu kwako na kuwe onyesho la shukrani kwa yote ambayo Muumba wako amekufanyia. Bibilia yatuimiza tumwimbie nyimbo za sifa, “Mfanyie BWANA shangwedunia yote,Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru, nyuani mwake kwa kusifu, Mshukuruni, limidi jina lake” (Zaburi 100:1, 4). Maisha yako yote yatengwe kwa utmishi wa Mungu. Vipawa vyako vyote, muda, raslimali lazima vitumike kwa utukufu wake. Yesu anena, “Msujudie Bwana Mungu wako, humwabudu Yeye peke yake” (Luka 4:8).

Kwabudu,shukrani na huduma vinafanyika kwa kutii Amri za Mungu. Bibilia yasema, “Mche Mungu, nawe uzishike Amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu” (Mhubiri 12:13). Jukumu lako lote kwa Mungu lapeanwa katika sheria za Mungu. Katika Amri kumi za Mungu,anatwambia anachohitaji kutoka kwetu. Sheria ya mungu yapatikana katika Bibilia,vifungu kumi na saba vya kwanza katika Kitabu cha Kutoka Mlango wa Ishirini.

Katika Amri Nne za kwanza, tunajifunza jukumu letu la pekee kwa Mungu.

 1. Uwe na Mungu mmoja pekee, Mungu wa kweli wa Bibilia. Yeye peke yake awe tegemeo la upendo wako na kwabudu kwako. Miungu mingine yote sio miungu ya kweli. Miungu ya dini zingine na miungu ya kujifuhisha, pesa, na mamlaka yote yakataliwe.

 2. Usiabudu mfano wowote kuwa Mungu,au usijifanyie mfano wa kwabudu.Mwabudu Mungu kwa kusikia na kutii mahubiri ya neon lake.

 3. Mungu ametukataza tusilitaje Jina lake bure, kwa kulaani, kuapa, na kulitumika jina lake isivyo stahili.Lazima uchunge kuogopa na kuliheshimu Jina lake takatifu.

 4. Mungu akuhitaji kuitunza siku ya Sabato (Jumapili). Ni siku takatifu. Usiitumie kufanya kazi yoyote ila tu kwa kwabudu na kumtumikia Mungu. Unahitajika kwend kanisani ambapo ukweli wa Bibilia unahubiriwa.

Mungua hajatuhitaji kuwa na tabia Fulani kwake, bali pia tuwatendee mazuri binadamu wenzetu. Majukumu haya yapatikana katika Amri sita za mwizo.

 1. Waheshimu baba na mama yako na wale wote wenye mamlaka juu yako, kama vile maafisa wa serikali na viongozi wa Kanisa na mwajili wako.Hayo yote hudihilika katika heshima, unyenyekefu na utiifu.

 2. Mungu amakataa chuki, kudhuru au kuua mtu yeyote hata wewe mwenyewe, Mungu amekataa choyo,hasira na kisasi. Lazima tuwapende adui zetu.

 3. Usifanye ngono na yeyote ambaye siye mke wako au mume wako kisheria.Mungu amekataa huasherati, katika moyo, tamaa ya moyo na mahitaji mabaya.

 4. Usiibe kitu chochote amabacho sio chako. Jipatie mahitaji kwa bidii yako mwenyewe.

 5. Usiwe shahid wa uwongo dhidi ya yeyote kwa mazengenyo, mazungumzo mabaya, mazungumzo yasio faidi. Uwongo wa aina yoyote umekataliwa.

 6. Usitamani moyoni chochote ambacho sio chako.

Lazima ijulikane kuwa Mungu haitaji tu utiifu wa nje bali pia utiifu wa moyo uchukie yale yote. Moyo wako lazima uchukie yale yote ambayo Mungu amekataa na kufurahia yote ya haki. Yesu afundisha kuwa sheria za Mungu zaweza kujumlishwa na kuwa neno moja, Upendo. Anasema, “Mpemde Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.Hii ndiyo Amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika Amri hizi mbili hutegemea torati na manabii” (Mathayo 22:37-40).

Mungu haitaji chochote ila upendo uliokamilika. Lazima tumpende na nafsi zetu zote. Upendo huwe chanzo cha heshima,kwabudu, shukrani and huduma.

 

Kushindwa Kwa Mwanadamu

Ukijua kuwa Mungu ndiye muumbaji wako, mhifadhi na mtawala ambaye anahitaji humpende, humwabudu na kumhudumia, lazima huelewe pia kitu kimoja cha msingi kukuhusu, wewe ni mwenye dhambi ambaye ameshindwa kutekeleza majukumu yake kwa Mungu. Hupendi, hauabudu wala kumtumikia inavyo kupasa. Hauchatunza Amri Kumi ulizo pewa na Mungu. Ingawa haujaasi baadhi ya Amri hizi nje, umevunja kila moja wazo ndani ya roho. Hauja mpenda mungu kwa moyo wako wote,roho yako yote na kwa nguvu zako zote. Maisha yako yote hayachatakaswa kwa kuabudu na kumtumikia Mungu. Wewe ni mtenda maovu na lazima useme, “nimefanya dhambi, nikufanyeje Ee Mlinda wanadamu? ...” (Ayubu 7:20). “Maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi …” (Ayubu 13:23), “Tazama mimi si kitu kabisa” (40:4). Ukikataa kuwa wewe si mwenye dhambi, unajidanganya na kumfanya mungu kuwa mwongo. Bibilia inasema, “Tukisema hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu” (1Yohana 1:8).

Watu wote ni sawa maana wote wametend dhambi.” Hakuna mwenye haki hata mmoja, hakuna hafamye, hakuna amtafutaye Mungu, wote wamepotoka, wameoza wote pia, hakuna mtenda mema, La! Hata mmoja” (Warumi 3:10-12). Hakuna hata mmoja, kila mmoja ameshindwa na jukumu lake kwa Mungu. Hata matendo yale ambayo huonekana kuwa mazuri sana sio mazuri kwa Mungu. Bibilia yasema, “Na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi” (Isaya 64:6). Mungu ataka ukamilifu lakini mwanadamu yu mbali nao.

Kushindwa kwetu kutimiza jukumu letu kwa Mungu sio makosa ya Mungu. Mungu alimuumba mwanadamu mwenye haki na uweza wa kufanya yote mungu aliitaji. Lakini baba wetu wa kwanza Adamu, alihasi kinyume na Mungu. Alimhasi Mungu na kuanguka kutoka haki hadi dhambini. Alipoanguka katika dhambi, ndani yake akawa mtend a maovu. Badala ya kumpenda, kumtumikia Mungu,alipenda dhambi na kumtumikia Ibilisi. Hali potovu ya Adamu ikafikia uzao wake wote. Kwa sababu sis ni wana wa Adamu, sis pia tumerithi hali yake potovu. “Kama kwa mtu mmoja dhambi ilingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti ikawafikia watu wote,kwa sababu wote wamefanya dhambi” (Warumi 5:12). Bibilia yaita hali hiyo hupotovu wa kiroho- kufa kiroho. Tunafanya dhambi kwa sababu ndani yetu tumepotoka. Tumekufa kiroho. Bibilia yazumngumzia hali ya ndani potovu ya mwanadamu, inasema, “Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote. Una ugonjwa wa kufisha,nani awezaye kuujua?” (Yeremia 17:9).

Hata hivyo, kushindwa kwetu kutimiza jukumu letu kwa Mungu hakujabadilisha ukweli kwamba hitaji la Mungu kwetu lina baki kuwa lilelile. Mungu hajabadilika. Anabaki kuwa Mungu Mtakatifu. Malaika wanaitana mbele zake wakisema, “Mtakatifu, Mtakatifu, Ndiye BWANA wa Majeshi” (Isaya 6:3). Mungu Matakatifu ni Mkamilifu, hatendi dhambi wala hapendezwi na dhambi za wengine. Mungu huchukia dhambi na wale watendao dhambi. Bibilia yamzungumzia Mungu, “Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya, mtu mwovu hatakaa kwako, wajivunao hawa tasimama mbele za macho yako, unwachukia, wote watenda ubatili, utawaharibu wote wasemao uongo, BWANA humzira mwuaji na mwenye hila” (Zaburi 5:4-6). Mungu ni mwenye wivu, Anasema,” Maana hutamwabudu Mungu mwingine, kwa kuwa BWANA ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu” (Kutoka 34:14).

Hata kama wewe ni mwenye dhambi bado wewe ni kiumbe wa Mungu na wivu, anakukataza kuwa na miungu mingine. Mungu wa wivu anakutaka humpende, humwabudu na kumtumikia Yeye peke yake.

Kwa sababu binadamu ameshindwa kutekeleza jukumu lake kwa Mungu,wote bila upendo wanastahili hukumu na huaribifu wa milele kutoka kwa mungu. Unastahili hukumu ya milele katika jehanamu. Mungu ni mwenye wivu kwa utakatifu wake na atamwadhibu yeyote atendaye dhambi. “BWANA ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi, BWANA hujilipiza kisasi naye ni mwingi wa hasira, BWANA hujilipiza kisasi ju ya adui zake, huwawekea adui zake hakiba ya hasira, BWANA si mwepezi wa hasira, ana uweza mwingi wala hamhesabii mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe …” (Nahumu 1:2-3).

Wakati wa mwisho Mungu atawapeleka ambao hawakuokolewa kwa neema yake, na wale wote wako katika hali ya dhambi jehanamu na mauti ya milele. Yesu anasema, “Ndivyo itakavyo kuwa katika mwish wa dunia, malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndip kutakuwa kilio, na kusaga meno” (Mathayo 13:49-50). Mbali na neema ya Mungu, hakuna kuepuka hukumu ya milele ambayo Mungu hujilipia kisasi ghadhabu.

 

Wokovu Wa Mungu

Hali ya Binadamu huonekana kuwa bila tumaini. Tutaepukaje ghadhabu ya Mungu na huaribifu wa milele katika Jehanamu? Je! Wenye dhambi watamjia mungu vipi ili wamjue kwa undani waishi na kuwa na ushirika na Yeye? Je! Mwenye dhambi atakuwa mtakatifu vipi? Kwa Binadamu haiwezekani, “Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kisicho kisafi? Hapana awezaye” (Ayubu 14:4). Lakini kisichowezekana kwa binadamu, kwa Mungu chawezekana. Muumba mwenye utukufu, Mhifadhi na Mtawala wa ulimwengu ni Mwokozi pia ambaye hukomboa kutoka dhambini, mauti na jehanamu. Mungu asema, “Mimi, naam, mimi ni BWANA, zaidi yangu mimi hakuna Mwokozi” (Isaya 43:11).

Mungu wa kweli si Mungu Mtakatifu tu na mwenye haki ambaye huukumu wenye dhambi, bali pia ni Mungu mwenye upendo na neema, ambaye huonyesha huruma, katika neema yake na upendo Amemtuma Yesus Kristo kutimiza wokovu, Mungu katika Yesu Kristo ndiye mwokozi pekee.

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu aishiye milele ambaye alishuka ulimwenguni na akajitweka ubinadamu. Yeye n i Mungu kweli, lakini pia ni mwanadamu kamili. Ndani ya Kristo, “Na bila shaka siri ya utauwa ni Kuu, Mungu alidhihilishwa katika mwili” (1Timotheo 3:16). “Nao watamwita jina lake Imanueli, yaani, Mungu pamoja nasi” (Mathayo 1:23). Yesus alijukuliwa mimba na Roho Mtakatifu akazaliwa na bikila Mariamu. Baada ya kuwa mtu mzima, Alihubir i Injili kwa miaka mitatu unusu. Aliwambia watu kuhusu Mungu ambaye hukoa wenye dhambi. Katika maisha yake yote, Alimpenda, kumtumikia na kumtii Mungu kikamilifu. Mwisho wa maisha yake Alijukuliwa na waovu akapelekwa Kalfari na akawambwa msalabani ambapo alikufa vile Mungu alikusudia tangu mwanzo. Baada ya siku tatu kaburini, alifufuka kutoka kwa wafu. Alipaa Mbinguni na sasa Ameketi katika mkono wa Kuume wa Mungu akiutawala ulimwengu hadi atakaporejea kuwahukumu walio hai na walio kufa.

Kwa kujitolea kwake kufa, Kristo Alipata wokovu. Wakati aliteseka na kufa msalabani, Alisijukua mwilini mwake dhambi sote za wale wote Mungu alichagua kuwaokoa, Kwa maana Kristi naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili Atulete kwa Mungu …” (1Petro 3:18). Alihesabiwa dhambi zao na Mungu akamtesa Kristo kwa niaba yao. Kristo alilipa deni walilo kuwa nalo kwa Mungu ili wapate msamaha wa dhambi zao. Tunasoma, “Ambaye katika Yeye (Kristo) tuna ukmbozi, yaani msamaha wa dhambi” (Wakolosai 1:14).

Zaidi ya hayo haki yote ya Kristo ikahesabiwa kuwa yao, kama wale ambao wamempenda, kumwabudu, kumtumikia na kumtii Mungu kikamilifu. Kristo Ametimiza hitaji la Mungu badala yao. “Kwa sababu kama kuasi kwa mtu mmoja (Adamu) watu wengi wameingiza katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja (Kristo) watu wengi wameingiza katika hali ya wenye haki” (Warumi 5:19). Kifo cha Yesu kikaokoa wenye dhambi kutoka kwa ghadhabu na hukumu ya Mungu. “Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” (Warumi 8:1).

Kristo hakupata wokovu kwa kazi yake msalabani, bali pia Anaudhilihisha katika maisha ya wale wote ambao Mungu Amechagua kuokoa ili kwa hakika wapate kuujua wokovu. Kristo huwafufua kutoka mauti ya kiroho na kuwafanya hai kiroho kwa kuwafanya wapya kiroho ili wampende. Kwa hivyo Mungu Asema, “Nami niwapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe, uliomo ndani ya mwili wenu, … Nami nitatia roho yangu ndani yenu na kuwahendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda” (Ezekieli 36:26-27), kutoka kwa moyo mpya, Kristo hutoa imani na toba ili mpya wa Mungu asiache dhambi zake na kwa imani amwabudu na kumhudumia Mungu wa kweli japo sio kwa ukamilifu. Anafikia kumjua Mungu kama mwokozi wake katika hali ya kindani na ya kipekee. Mungu anatembea naye, anaongea naye na kuwa na ushirika pamoja naye, “Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue Yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake aliye wa kweli yaani ndani ya Mwana wake Yesu Kristo, Huyu ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele” (1Yohana 5:20). Kristo huwaleta waaminio katika ushirika pamoja na Mungu wa kweli na haishiye. Wokovu hu si kazi ya mwanadamu. Hatuwezi kufikilia, kusema au kufanya chochote kupata wokovu huu. Ni kazi ya Mungu peke yake. Bibilia yasema hivi kumhusu,” Ambaye Ametuokoa Akatuita kwa mwito Mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisis, bali kwa kadiri ya makusudi yake Yeye na neema. Neema hiyo tulipewa katika Yesu Kristo …” (2Timotheo 1:9). Mungu huokoa kwa neema yake pekee. Wokovu si kitu tunacho stahili. Ni kipawa ambacho tunapokea bure kupitia Kristo Yesu. “Kwa maana mumeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu, wala si kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9). Mtu awaye yote asije akajisifu kuwa alichangia chochote kupata wokovu. Wokovu “si kwa uweza wa yule atakaye, wala kwa yule apigaye mbio,bali kwa Yule arehemuye yaani Mungu” (Warumi 9:16).

 

Imani Ya Kweli

Kwa vile mungu huokoa kwa kupeana imani kwa mwenye dhambi, wokovu hautawezekana bila imani. Bila imani hakuna yeyote ataitwa mwan wa kweli wa Mungu. “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza (Mungu) …” (Waebrania 11:6). “Amwaminiye Mwana yu na uzima wa milele, asiye mwamini Mwana hataona uzima bali ghadabu ya Mungu inamkalia” (Yohana 3:36). Je! Wataka kuiepuka ghadabu ya Mungu na huaribifu wa milele katika jehanamu? Je! Umelemewa na mzigo wa dhambi zako na watafuta msamaha? Je! Watamani kumjua Mungu na Mwanawe Yesu Kristo na hufurahie uzima wa milele? Yesus asema, “Mwamini Mungu” (Mariko 11:22). Mtu mmoja aliuliza, “Nifanyeje nipate kuokoka?” Alijibiwa, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako” (Matendo Ya Mitume 16:30-31). Mungu anatuitaji twaamini.

Imani Ya Kweli Ni Ipi? Imani ni vitu vitatu:

 1. Ni ufahamu wa kweli Fulani kumhusu Mungu,Kristo, binadamu na wokovu.

 2. Ni kutanbua kuwa ukweli huu ni wa kwaminiwa.

 3. Ni kusadiki na kumtegemea Mungu wa kweli na Mwanawe Yesu Kristo kama mwokozi wako.

Je! Twaamini Yapi?

 1. Lazima twaamini kuwa mungu ndiye Muumba mkuu, Mhifadhi na Mtawala wa ulimwengu. Tunamtegemea kwa vitu vyote.

 2. Lazima twaamini kuwa ni jukumu letu kumpenda, kumwabudu, kumtumikia na kumtii Mungu.

 3. Lazima twaamini kuwa sisi ni wenye dhambi ambao hawawezi kutimiza wajibu wao kwa Mungu. Tunastahili mateso katika jehanamu ya milele.

 4. Lazima twaamini kuwa mungu alimpeleka Mwanawe wa pekee Yesu Kristo kuwaokoa wenye dhambi. Kristo alikamilisha wokovu kwa kufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamana. Siku ya tatu alifufuka kutoka kwa wafu kwa ushindi mkubwa kama Mwokozi.

 5. Lazima twaamini kuwa Mungu katika Kristo Ndiye Mwokozi anaye tukomboa kutoka kwa dhambi zetu na kutupatia uzima wa milele.

Toba Ya Kweli Ni Vitu Vitatu:

 1. Ni kukubali kuwa sisi hakika ni wenye dhambi wanaohitaji wokovu.

 2. Ni kujutia dhambi. Hatuombolezi juu ya matokeo ya dhambi zetu. Tunajuta kuwa tumetenda dhambi kinyume na Mungu muumba wetu, Mhifadhi na Mtawala.

 3. Ni kujitenga na dhambi zetu na kuchuana nazo. Tusitamani ten kuishi maisha ya uovu, bali tumtafute Mungu na haki yake.

Imani ya kweli hujaza moyo wa aaminiye na shukrani ya kutaka kumtii Mungu. Inamfanya kutanbua vile Mungu alivyo wa ajabu kwa kumwokoa dhambini.Anampenda Mungu na kutamani kufanya yote ambayo Mungu Amemwamuru.Hata ingawa hatii Amri za Mungu kikamilifu atamani kutunza Amri zake.

Yesu Asema, “Mkinipenda mtazishika Amri zangu” (Yohana 14:15). Muumini wa kweli ataonyesha upendo wa Mungu kwa hatua ya imani kwend kanisani kuhudhulia ibada mahali atasikia mahubiri ya neno la mungu, Bibilia. Atasoma na kujifunza Bibila nyakati zote, ataenda mbele za Mungu wake kwa maombi kila siku, Atahitaji kumjua Mungu zaidi na zaidi,kwa vile ajua mwanzo mdogo wa hekima ya Mungu.Sehemu kubwa ya maisha yake ataitoa kwa kujifunza zaidi kuhusu Mungu wa kweli na Mwanawe Yesu Kristo.

Mtu ambaye an imani ya kweli hafikilii kuwa imani yake, toba na utiifu ni kazi yake mwenyewe. Hafikilii kuwa hizi ni sehemu yake katika wokovu, ionekane kuwa amemzaidia Mungu kuupata. Anajua na kwamini kuwa hivi vyote ni sehemu ya wokovu ambao Mungu amepatiana bure kama kipawa. Hangekuwa na imani, toba, upendo na utiifu bila neema ya Mungu ambayo inafanya kazi pamoja na hizi ndani ya mpyo wake na maishani mwake. Yesus Asema, “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote” (Yohana 15:5). Au hafikilii kuwa kwa imani yake, toba, upendo na utiifu anatimiza hitaji la Mungu peke yake. Anaamini kuwa wokovu wake unategemea kabisa kufa na kufufuka kwake Yesu Kristo.

 

Wamjua Mungu Wa Kweli?

Je! Wamjua Mungu wa kweli na Mwanawe Yesu Kristo? Je! Wajua Baraka itokanayo na uzima wa milele? Kama sio Mungu Akwamru, “Na hii ndiyo Amri yake,kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo …” (1Yohana 3:23). Ikiwa umeamini tayari, mtafute na kumjua Mungu zaidi pamoja na Mwana wake.

Yesu Asema, “Na izima wa milele ndio huu,wakujue wewe Mungu wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.”

Ikiwa una maswali yoyote kuhusu hayo umeyasoma, au ikwa ungependa kujua zaidi kumuhusu Mungu, wasiliana nasi kwa habari zaidi.